Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 24Article 559516

Uhalifu & Adhabu of Friday, 24 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mshtakiwa Kesi ya Mbowe "Nilining'inizwa Kama Mshikaki"

Mbowe na wenzake wakiwa mahakamani. Mbowe na wenzake wakiwa mahakamani.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi namba 16/2020 ya uhujumu uchumi na ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya mahakama hiyo kufunga ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Hayo yamejiri leo Ijumaa, Septemba 24, 2021 baada ya Jaji anayesikiliza kesi ya hiyo Mustaphe Siyani kuridhia kwamba ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ufungwe hivyo akaruhusu kesi ya msingi kuendelea ambapo mshatikiwa namba mbili, Adam Kasekwa ameanza kujitetea.

Akiongozwa na wakili wa Utetezi, John Mallya, shahidi huyo ameleza namna alivyokamatwa na Polisi akiwa mkoani Kilimanjaro, ambapo amedai akiwa eneo la Rau Maduka alivamiwa na kikundi cha Askari Polisi na kuanza kupigwa huku akiwekewa madawa ya kulevya kwenye mfuko wake wa suruali Pamoja na silaha.

Aidha, mshitakiwa amedai kwamba akiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi (Central) katika nyumba iliyokuwa pembezoni mwa kituo alivuliwa nguo zote na kuning’nizwa kwenye chuma kama mshikaki au popo kisha akaanza kusurubiwa.

Ameendelea kuieleza mahakama kwamba akiwa katika Kituo cha Polisi Mbweni alikopekwa bila yeye kujua anakoelekea baada ya kuginwa na jacket usoni aliamriwa kubadili jina lake na kuitwa Vicent Juma aliyekamatwa kwa kosa la unyang’anyi mkoani Tabora.

Kasekwa ameiambia mahakama kuwa wakati wa ukamatwaji wake huko Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo miongoni mwa waliomkamata ni ACP Kingai ambaye kwa sasa ni RPC wa Kinondoni kwa sasa ambaye kwa wakati huo alikuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, alichukua fedha zake alizokuwa nazo mfukoni ambazo zilikuwa ni shiling 160,000 ambazo mpaka sasa hajui zilipo.