Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552484

Habari Kuu of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Msipochanja mtakufa, waume zenu wataoa wanawake wengine" - Waziri Gwajima

Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Dorothy Gwajima amewatahadharisha Wanawake kuhusu kuchanja chanjo ya COVID-19 kwa kuwa wasipochanja wakiumwa watakufa na wanaume zao wataoa wanawake.

Amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo kwani wanawake ndio nguzo ya familia, ikiwa ni pamoja na kuepuka upotoshaji unaoendelea katika mitandao ya kijamii kuwa chanjo hiyo, ni ishara ya siku za mwisho.

"Wadada wazuri mliopo hapa mtaawacha waume zenu, alafu unamwachia nani mume wako, ataoa!kisha mnaniongezea mzigo wa watoto wa kambo, watoto yatima kisa mama katangulia mbele za haki? wanaume wamejanjaruka wanachanja, muache imani potofu, namba 666, haiwezi kufanya kazi hadi kanisa linyakuliwe, kwani kanisa limenyakuliwa?

Amefafanua kuhusu tuhuma zinarushwa juu yake kuhusu kubadilika kwa mitazamo yake juu ya mapokeo ya chanjo, kuwa chanjo ni sayansi na kama kuna swali kuhusu chanjo hiyo basi wawaulize wataalamu wa afya.