Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540739

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Mtaka ataka maonyesho yenye hadhi ya makao makuu

Aidha, amesema ofisi yake itaanzisha kitengo cha uatamizi kwa ajili ya kulea, kuendeleza na kuzitumia bunifu mbalimbali.

Aliyasema hayo juzi katika maonyesho ya pili ya vyuo vya elimu ya ufundi yaliyoandaliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), yanayofanyika jijini hapa.

Alisema mkoa huo upo tayari kuwalea na kukuza wabunifu ambao watakuwa wamebuni teknolojia mbalimbali kupitia kwenye maonyesho husika.

“Wakati tunapohitimisha maonyesho haya, Mtendaji Mkuu wa NACTE, tufanye kikao cha pamoja, nimeona hapa kuna vijana wamebuni teknolojia kwenye mita za maji, kwenye kuzuia pancha za magari wakati yanapokuwa yanatembea, kama serikali huu ubunifu tunapaswa kuulea hata kuununua,” alisema.

Alisema anatarajia kukutana na viongozi wa taasisi mbalimbali zilizoshiriki maonyesho ya NACTE kwa ajili ya kufanya mazungumzo ikiwamo kupata kalenda ambazo zinaonyesha kuna matukio ya aina gani, ili kusaidia kuandaa maonyesho yenye taswira ya makao makuu.

Aliiomba NACTE kuhakikisha mwakani mkoa unakuwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano hayo, ili kusaidia kutangaza maonyesho hayo.

“Natarajia kukutana na taasisi zote zinazoandaa maonyesho, nahitaji kuona tunafanya nini ili tuweze kuifanya Dodoma kuonekana ni makao makuu kama ilivyo miji mingine ya nje ya Tanzania,” alisema Mtaka.

Alisema anaamini kwamba maonyesho hayo na yajayo yakiboreshwa yatabadili taswira na kuchangamsha biashara ya mkoani hapo.

“Naamini tukifanya hivyo tutafika mbali na kubadilisha taswira ya maonyesho ambayo yatakuwa na tija na faida kubwa kwa wananchi na washiriki,” alisema Mtaka.

Aliwaomba waandishi wa habari kuhakikisha wanashirikiana na NACTE au taasisi nyingine zozote kuhakikisha wanayatangaza maonyesho hayo kwa siku zilizobaki ili jamii ijue na kujitokeza kutembelea na kujifunza.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Adolf Rutayuga, alisema mkuu huyo amekagua maonyesho katika mabanda zaidi ya 150 na kutoa ushauri vitu vya kuboresha.

Join our Newsletter