Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 19Article 572656

Habari Kuu of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mtoto wa Miaka Sita Aingiliwa na 'Baba Mdogo'

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa

KATIKA hali ya kustaajabisha, mtoto wa miaka sita (jina linahifadhiwa) katika Kata ya Nyombo, Manispaa ya Njombe amebainika kuingiliwa kimwili na kuharibiwa sehemu zake za siri na mtu aliyetajwa kuwa ni baba yake mdogo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema mtoto huyo ambaye huishi na bibi yake, majira ya jioni bibi huyo hutoka kwenda kwenye vilabu vya pombe kujiburudisha na kurejea nyumbani usiku.

Hivyo baba mdogo huyo hutumia mwanya huo ambao bibi hayupo na kumwingilia mtoto huyo na kumfanyia ukatiri wa kingono mara kwa mara.

Kamanda Issa amesema baada jeshi la polisi kupewa taarifa hizo lilifanya uchunguzi na kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, lakini uchunguzi wa madaktari nao ulithibitisha kuwa ni kweli binti huyo alikuwa akiingiliwa kimwili na ameharibiwa sehemu zake za siri. Mpaka sasa mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.