Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552145

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Muhitimu chuo kikuu awaburuza Bodi ya Mikopo Mahakamani

Kesi dhidi ya Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu Kesi dhidi ya Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu

Mhitimu wa chuo kikuu cha Tumaini Makumira Arusha, Alexanda Bakunguza, amefungua kesi Mahakama Kuu, dhidi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) akipinga kugharamiwa na Serikali kwa njia ya mkopo.

Anadai kuwa tozo na riba zilizopo katika mikopo wanayopewa ni kubwa hivyo inamchelewasha mwanafunzi kupata maendeleo pamojna na kuwa kaelimika.

Muhitimu huyo ameitaka serikali kugharamia masomo pasi kumlipisha mwanafunzi gharama yoyote ile.

Amefafanua kwa kutumia Ibara ya 11 katika katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inaeleza kuwa serikali itafanya jitihada kubwa kuhakikisha watu wote wanapata fursa sawa za mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za ashule na vyuo.

kesi hii namba 16, ilifunguliwa julai 29, mwaka huu na inasimamiwa na jopo la majaji watatu huku Mawakili kutoka shirika kutetea haki za bianadamu LHRC wakiwa tayari kwa ajili ya kutoa Tambo za kisheria katika usimamizi wa madai ya Muhitimu huyo.