Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 574018

Habari Kuu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: bbc swahili

Mume na mke wake wakamatwa kwa kuwauza watoto wao

Mume na mke wake wakamatwa kwa kuwauza watoto wao Mume na mke wake wakamatwa kwa kuwauza watoto wao

Vikosi vya usalama vya vya ulinzi wa raia nchini Nigeria vimemkamata mwanaume mmoja kwa jina , Elisha Effiong, kwa madai ya kupanga njama na mke wake ya kuwauza watoto wao wawili pesa za Nigeria - N700,000 (dola 1707) katika jimbo la kusini mwa nchi hiyo laAkwa Ibom.

Gazeti la Vanguard limechapisha taarifa ya msemaji wa kamishna wa polisi Umana Ukeme Jumatano, akisema kuwa binti zao waliotaka kuwauza walikuwa na umri wa miaka sita na miaka minne.

Kulingana naye, Effiong, ambaye anaishi nchini Cameroon na mke wake walikamatwa katika eneo la Uyo tarehe 15, 2021,kufuatia taarifa iliyotolewa kwa siri huku wakijaribu kuwauza watoto wao Abasifreke Edet na Rachael Edet .

Taarifa hiyo imemnukuu mshukiwa akisema alitaka kuwauza watoto wake kwasababu ya umasikini mkubwa alionao.