Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 16Article 557995

Habari Kuu of Thursday, 16 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Muongozo mpya wa wasafiri nchini kuanza Septemba 19

Muongozo mpya wa wasafiri nchini kuanza Septemba 19 Muongozo mpya wa wasafiri nchini kuanza Septemba 19

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar kupitia wizara zenye dhamana ya Afya zimekubaliana kwa pamoja kuanza kutumika kwa mwongonzo wa wasafiri namba nane kuanzia ktuumika kuanzia Septemba 19.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa serikali, Dk Aifelo Sichwale ambapo alisema mwongozo huo utazingatia upimaji afya wasafiri wanaoingia nchini na upimaji Corona kwa kutumia kipimo cha haraka cha Covid 19 Rapid Antigen Test (C19RAT) kwa baadhi ya wasafiri wanaotoka katika nchi zenye maambukizi makubwa kulingana na mwenendo wa ugonjwa kwenye nchi wanazotoka.

Alisema katika kuhakikisha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko yanayosambaa kwa kasi duniani, serikali ilitoa mwongozo wa wasafari ndamba saba Mei 14, 2021.

Alisema kutokana na tathmini ya hali ya maambuki ya Corona duniani na mahitaji ya upimajji wa ugonjwa huo nchini, serikali imehusisha mwongozo namba saba na kutoa toleo namba nane.

Alisema kutokuhitajika kwa cheti za RT – PCR wala kipimo cha C19RAT kwa watoto chini ya miaka mitano, wafanyakazi wa ndani ya ndege, abiria wanaounganisha safari, madereva wa magari ya mizigo wote watapima kipimo cha haraka bila malipo wanapoingia nchini.

Aidha alisema abiria wanaoingia nchini kupitia usafiri wa nchi kavu watawajibika kuwaslisha cheti halali cha kuthibitisha kuwa hawana maambukizi ya Covid 19