Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552115

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Muuguzi apigwa faini Tsh. laki tano kwa kesi ya Rushwa

Muuguzi apigwa faini Tsh. laki tano kwa kesi ya Rushwa Muuguzi apigwa faini Tsh. laki tano kwa kesi ya Rushwa

Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemhukumu muuguzi aliyekuakifanya kazi katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Wallace Kaziri (53) kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh 500,000.

Kaziri alipatikana na hatia ya makosa matatu likiwamo la kuomba na kupokea rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa mgonjwa. Mshitakiwa alilipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Akitoa hukumu hiyo jana Agosti 17, Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Godfrey Rwekit alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine ambao wanapenda kuomba rushwa bila kujali madhara yake.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Igunga, Mazengo Joseph alidai Kaziri alishitakiwa kwa makosa matatu ya rushwa.

Alidai katika shitaka la kwanza, Oktoba 30, 2019 akiwa muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Kaziri aliomba rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa Kasemba Bundala.

Alidai Bundala aliombwa rushwa ili Kaziri ampatie Bugumba Luhende dawa za kifua kikuu. Alidai Luhende ni mama wa Bundala na alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo.

Katika shitaka la pili, alidai Oktoba 30, 2019, Kaziri alipokea kiasi cha Sh 50,000 kwa njia ya simu kama malipo ya awali ya Sh 200,000 alizoomba.

Mazengo pia alidai kuwa, Novemba Mosi, 2019 Kaziri alipokea Sh 50,000 zikiwa ni malipo mengine kati ya Sh 200,000 alizoomba awali, hivyo akawa amepokea jumla ya Sh 100,000.

Mshitakiwa alikana kutenda makosa hayo. Upande wa Jamhuri umepeleka mahakamani mashahidi tisa na vielelezo 12.