Uko hapa: NyumbaniInfos2020 09 25Article 510337

Crime & Punishment of Friday, 25 September 2020

Chanzo: Millard Ayo

Mwalimu aliekatwa na panga na mwanafunzi "nikaona tu mkono unaning'inia"

Mwalimu aliekatwa na panga na mwanafunzi "nikaona tu mkono unaning'inia"

Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia mwanafunzi wa Kidato cha tatu Mwita Machamo,(17) wa shule ya sekondari ya Kiagata kwa kumkata na panga mwalimu wake Majogoro John, baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kumpeleka mzazi wake shuleni kama alivyoagizwa na mwalimu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Daniel Shillah amesema kuwa tukio hilo lilitokea shuleni hapo majira ya asubuhi wakati mwalimu anakagua wanafunzi watoro, na ndipo mwanafunzi huyo alimgeukia mwalimu wake na kumkata mapanga.

“Baadhi ya wanafunzi waliwaleta wazazi wao, lakini huyu mwanafunzi kwa utovu wa nidhamu uliopindukia alikuja na upanga akiwa ameuficha kwenye nguo zake na mwalimu alipohoji kwanini hujaja na mzazi, mwanafunzi akachomoa upanga na kumshambulia mwalimu na akawatisha tisha wanafunzi wengine akapata nafasi ya kukimbia lakini wakamkata na tumemshikilia na atafikishwa mahakamani” Kamanda Shillah

Majogoro John ni mwalimu aliyejeruhiwa  “Nilipita darasani kuangalia watoro nikamuambia fuata mzazi tuje tuongee ili nijue shida nini yule akatembea hatua kama tatu kwenda mlangoni akageuka alivyotoa upanga akageuka haraka akanikata begani akageuka tena ili anikate kichwani ndio nikaweka mkono wa kushoto akapiga panga nikaona tu mkono unaning’inia”.

TAJIRI NAMBA 1, TRILIONEA, ALIGAWA DHAHABU KAMA PIPI, WALINZI ELFU 60, MSAFARA TEMBO 100, NGAMIA 80

Join our Newsletter