Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 23Article 559147

Diasporian News of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mwamko wa chanjo Zanzibar wampa furaha Rais Mwinyi

Mwamko wa chanjo Zanzibar wampa furaha Rais Mwinyi Mwamko wa chanjo Zanzibar wampa furaha Rais Mwinyi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema licha ya janga la ugonjwa wa Covid-19, kuna mwamko mkubwa wa watu wanaotaka kwenda kuwekeza visiwani humo.

Dk Mwinyi alisema jana kuwa wawekezaji wengi wamevutika na kuonesha nia ya kwenda kuwekeza Zanzibar hasa kwenye visiwa vidogovidogo, baada ya serikali kuvitangaza visiwa hivyo kwa ajili ya utalii.

Alisema hayo Ikulu Zanzibar alipokutana na kuzungumza na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

Taarifa ya Kitengo cha Habari Ikulu, Zanzibar ilieleza kuwa Dk Mwinyi alisema serikali itaendelea na juhudi za kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta manufaa kwa wananchi na kuimarisha uchumi.

Dk Mwinyi alimpongeza Ndugai kwa ziara yake Zanzibar iliyoanza Septemba 20 mwaka huu, akianzia katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na anatarajia kumalizia katika Mkoa wa Kusini Unguja kesho.

Kwa upande wake, Ndugai alimpongeza Dk Mwinyi kwa uongozi wake na kwamba wananchi wa Zanziba wana matarajio makubwa.