Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554548

Siasa of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mwana FA Afunguka Alivyonusurika Kwenye Ajali Usiku

mbunge wa muheza mwana fa kushoto akiwa na wahiba wake Ay play videombunge wa muheza mwana fa kushoto akiwa na wahiba wake Ay

Mbunge wa jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA, amepata ajali ya gari eneo la Mkambalani mkoani Morogoro jana Agosti 30, 2021 majira ya saa 2 usiku.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslim na kueleza kuwa mbunge huyo yupo salama.

Kwa upande wake Mwana FA alipopata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari alieleza kuwa kabla ya ajali waliona gari mbele yao inataka kupita gari (Overtake) na ilikuwa mwendokasi sana hivyo hawakuweza kuikwepa ndio ikawaparamia.

Aidha amesema kiafya yeye na mwenzake aliyekuwa naye kwenye gari ni wazima ila alikuwa anasikia maumivu kidogo kifuani mwake.