Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 12Article 585124

Habari za Mikoani of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mwanafunzi UDSM afariki kwa kujirusha ghorofani

Mwanafunzi UDSM afariki kwa kujirusha ghorofani Mwanafunzi UDSM afariki kwa kujirusha ghorofani

Mwanafunzi mmoja aitwaye Manawa Samson Horera (22) ambaye ni Mwanafunzi wa mwaka wa pili kitivo cha shahada ya uhasibu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) amefariki baada ya kuruka kutoka ghorofa ya pili.

“Mwanafunzi huyo aliingia kwenye chumba cha Mwanafunzi mwenzake aitwaye Hamza Abdulhaman na kuiba laptop aina ya HP ambapo Hamza na Wanafunzi wengine wakamuona na alipobaini ameonekana na Wanafunzi wenzake aliamua kuruka kupitia dirishani”

“Jeshi la Polisi linawataka Wanafunzi kuacha kujihusisha na uhalifu kwani maeneo hayo ya hosteli yamekuwa na malalamiko ya Wanafunzi laptop zao kuibiwa na Watu wanaodhaniwa ni Wanafunzi wenzao suala ambalo linaweza kukatisha masomo yao ikibainika ni Wahalifu” ——— Muliro Jumanne, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM