Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 05Article 541180

Habari Kuu of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Mwanafunzi avaa maboksi akipinga combination aliyochaguliwa (+picha)

Mwanafunzi avaa maboksi akipinga combination aliyochaguliwa (+picha) Mwanafunzi avaa maboksi akipinga combination aliyochaguliwa (+picha)

Mwanafunzi Josephat John, aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo Manispaa ya Shinyanga, amezua taharuki ya aina yake Mjini Shinyanga mara baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango na kujifunika maboksi yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya Economics, Commerce , Accounts (ECA) ambayo amedai hawajawahi kuyasomea kwani yeye amesomea masomo ya Physics, Chemistry, Biology (PCB).Ametumia mbinu hiyo  ya kuvaa mabango kuiomba Wizara husika ifanye uchaguzi upya wa michepuo ili akasomee masomo ambayo ameshayasoma.Tukio hili limekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu atangaze matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kwenda vyuo vya ufundi na vyuo vya kati na kidato cha Tano mwaka 2021.

Join our Newsletter