Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 06Article 583624

Habari Kuu of Thursday, 6 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mwanafunzi wa Sekondari Avae Hata Sare ya Shule ya Msingi

Mwanafunzi wa Sekondari Avae Hata Sare ya Shule ya Msingi Mwanafunzi wa Sekondari Avae Hata Sare ya Shule ya Msingi

Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, ameendelea kusisitiza kwamba wakuu wa shule kutoweka vikwazo kwa wanafunzi wataokuwa hawana sare za shule badala yake wawaruhusu kuingia darasani hata na sare zao waliuzokuwa wanavaa shule ya msingi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januri 6, 2021, wakati akitoa tamkoa maalum kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo Januari 17, huku akimshukuru Rais Samia kwa kuwezesha ukamilikaji wa madarasa 12,000 nchini.

"Nimewaita hapa kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma kuhusu hali ya uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Awali, Darasa la Kwanza na mandalizi ya kuwapokea wa Kidato cha Kwanza kabla ya kufungua Shule za Msingi na Sekondari tarehe 17 Januari, 2022.

"Takwimu za maoteo ya uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Awali zinaonesha kuwa jumla ya Wanafunzi 1,363, 834 (Wavulana 676,028 na Wasichana 687,806) wanatarajiwa kuandikishwa ikilinganishwa na idadi ya Wanafunzi 1,198,564 (Wavulana 604,995 na Wasichana 593, 569) walioandikishwa 2021, Idadi hii inajumuisha Wanafunzi wenye mahitaji maalum 6,376 wakiwemo Wavulana 3,277 na Wasichana 3,099.

"Uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Awali ulianza Novemba, 2021 na unaendelea, hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2021 jumla ya Wanafunzi 488,780 wa Darasa la Awali wakiwemo Wasichana 247,003 na Wavulana 241,777 sawa na asilimia 35.93 ya Wanafunzi wote wanaotarajiwa kuandikishwa Darasa la Awali, waliandikishwa katika Shule za Serikali, idadi hii, inajumuisha Wanafunzi wenye mahitaji maalum 1,232 ambapo Wasichana ni 642 na Wavulana 590"

"Kama ni mwanafunzi wa sekondari anaweza akatumia sare yake aliyokuwa anavaa shule ya msingi wakati mzazi anatafuta fedha au akavaa tu t-shirt na sketi yake nzuri akaenda darasani, wazazi pia waangalie joining instruction (maelekezo ya kujiunga na shule) inasema nini kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo havina hata umuhimu, jamani tuondoe vikwazo," amesema Waziri Ummy.