Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 18Article 547339

Habari Kuu of Sunday, 18 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mwekezaji apongezwa kuzalisha umeme wa jua

Mwekezaji apongezwa kuzalisha umeme wa jua Mwekezaji apongezwa kuzalisha umeme wa jua

SERIKALI imesema itashirikiana na mwekezaji wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD kilichopo mkoani Kigoma kuhakikisha anafi kisha uzalishaji wa megawati tano kama ilivyokubalika kwenye mkataba uliosainiwa.

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato alisema hayo juzi alipotembelea kituo hicho kinachozalisha umeme megawati 1.8 zinazopelekwa kwenye kituo cha umeme cha Shirika la Umeme (Tanesco) mkoa wa Kigoma.

Alimpongeza mmikiki wa kituo hicho kwa hatua aliyofikia na kuahidi kuwa wizara hiyo itashirikiana nae ili kuhakikisha anafikisha uzalishaji wa megawati tano kama ilivyokubalika kwenye mkataba.

Alisema Tanzania ni nchi mojawapo inayoweza kunufaika na vituo vya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua kwa sababu inapata mwanga wa jua kwa kipindi kirefu katika mwaka.