Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552217

Habari za Mikoani of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mwenge wa Uhuru Kupitia Miradi yenye thamani ya Bilioni 105.1 DSM

Mwenge wa Uhuru Mwenge wa Uhuru

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amepokea Mwenge wa Uhuru leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIC), ukitokea Pwani na kuukabidhi wilaya ya Ilala kwa ajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo.

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa RC wa Pwani, Abubakar Kunenge, RC Makalla amesema kwa siku tano ambazo Mwenge wa Uhuru utakuwa Dar es salaam utapitia miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Shillingi Billion 105.1.

Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi kukimbizwa leo mkoani Dar es salaam. Utapita Ilala, kisha Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na kumaliza mbio zake Temeke. Agosti 23 Mwenge wa Uhuru utaondoka Dar es Salaam kuelekea Lindi.