Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 30Article 554449

Habari Kuu of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mwenyekiti wa TCD, Ztto Kabwe afanya ziara vituo vya Haki za binadamu

Mwenyekiti wa TCD, Zitto Kabwe, akiwa na viongozi wa LHRC Mwenyekiti wa TCD, Zitto Kabwe, akiwa na viongozi wa LHRC

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe leo amefanya ziara katika Ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), Ofisi za Foundation for Civil Society (FCS) pamoja na Legal Services Facility (LSF). Katika ziara hiyo Zitto aliambatana na Afisa wa TCD, ndugu Lucy Agostino.

Lengo la ziara husika ni uongozi mpya wa TCD kujitambulisha kwa wakuu wa taasisi hizo pamoja na kuona namna nzuri ya kushirikiana na LHRC, FCS na LSF katika jitihada za kuwezesha TCD kufanya kazi vizuri kufufua demokrasia na kutoa nafasi ya mijadala kati ya vyama vya siasa, serikali na asasi za kiraia.

Zitto alikabidhiwa majukumu hayo Agosti 26, 2021 kutoka kwa Mwenyekiti wa zamani James Mbatia, jijini Dar es salaam.