Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551305

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mwenyekiti wa makampuni ya ASAS afariki dunia

Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri

Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri amefariki dunia leo Ijumaa Agosti 13 alfajiri, akiwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia hiyo, Mzee Abri ambaye ni baba mzazi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Abri Asas, maziko yatafanyika leo baada ya Swala ya adhuhuri katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

"Hakutakuwa na mikusanyiko kwa tutakaokuwa Iringa, tafadhali tutumie zaidi teknolojia za habari kutoa pole na shughuli nyingine," ilieleza taarifa hiyo.

Mfanyabiashara wa Tanzanite, kada wa CCM afariki

Mwenyekiti wa CCM, Manispaa ya Iringa Said Rubeya alithibitisha taarifa hiyo na kutoa pole kwa familia, wafanyakazi wa Asas, ndugu jamaa na marafiki.

"Kama tulivyo shauriwa tutumie teknolojia ya habari na mawasiliano kuomboleza, nitoe pole nyingi kwa familia, pole pia kwa M NEC wetu, Salim Asas. Hakika kwa Mwenyezi Mungu ni marejeo," alisema Rubeya.