Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541441

xxxxxxxxxxx ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mwigulu kuanika bajeti ya Serikali Alhamisi

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba Alhamisi wiki hii anatarajiwa kuwasilisha bungeni Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Bajeti hiyo inatarajiwa kuwasilishwa sambamba na bajeti za nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

EAC ina wanachama sita ikiwemo Tanzania, Uganda, Rwanda, Kenya, Burundi na Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolea na Ofisi ya Bunge jijini Dodoma, kabla ya Dk Mwigulu kusoma bajeti hiyo kuanzia saa 10.00 jioni, asubuhi kuanzia saa 4.30 atawasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa nchi.

Leo Dk Nchemba anatarajiwa kuwasilisha bungeni bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango na itajadiliwa kwa siku moja.

Kesho na keshokutwa serikali inatarajiwa kushauriana na Kamati ya Bajeti na kufanya majumuisho kwa kuzingatia hoja zenye maslahi kwa taifa zilizojitokeza wakati wa kujadili bajeti za wizara.

Ushauriano wa serikali na kamati ya bajeti unafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Namba 124 (1) zilizofanyiwa marekebisho na kuanza kutumika Juni 2020.

Kama ilivyo desturi ya Bunge, tangu leo hadi Ijumaa kutakuwa na maswali ya wabunge kwa serikali.

Join our Newsletter