Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 573940

Habari Kuu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mwili wa Baba Yake Bashe Wawasili na Kuzikwa Usiku Nzega

Mwili wa Baba Yake Bashe Wawasili na Kuzikwa Usiku Nzega Mwili wa Baba Yake Bashe Wawasili na Kuzikwa Usiku Nzega

MWILI wa Marehemu Sheikh Mohamed Bashe umepumzishwa usiku wa kuamkia leo katika Makuburi ya Waislamu Kitongo Mjini Nzega Mkoani Tabora.

Akizungumza kwa niaba ya familia Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ambaye ni mtoto wa marehemu amesema familia inashukuru mchango wa jamii ya wakazi wa Nzega kwa namna walivyojitokeza kushiriki na familia katika mazishi hadi maziko ya baba yake.

Kabla ya mazishi imefanyika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Sheikh Bashe iliyoswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa mjini Nzega.

Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo mawaziri wamefika nyumbani kwa Naibu Waziri Bashe mjini Nzega ambapo wamejumuika pamoja na waombolezaji wengine kuupokea mwili huo.

Sheikh Mohamed Bashe alifariki Novemba 23, 2021 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.