Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540358

Habari Kuu of Friday, 28 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Mwinyi asimulia mauaji ya kimbari Rwanda yalivyompa wakati mgumu

Mwinyi asimulia mauaji ya kimbari Rwanda yalivyompa wakati mgumu Mwinyi asimulia mauaji ya kimbari Rwanda yalivyompa wakati mgumu

Anasema eneo la Maziwa Makuu, hususan mgogoro katika nchi za Burundi na Rwanda, ulisababisha aitishe mkutano kutafuta amani kwa nchi hizo, Aprili 6, mwaka 1994 jijini Dar es Salaam.

Kwenye simulizi ya kitabu chake kiitwacho ‘Mzee Rukhsa. Safari ya Maisha Yangu’, Mzee Mwinyi, anasimulia namna alivyoweka jitihada za kutafuta amani na usalama kwa juhudi zake na kushirikiana na viongozi wenzake.

“Mojawapo ya mambo yahusuyo nchi za nje yaliyonisumbua sana wakati nikiwa rais ni matatizo ya maeneo ya Maziwa Makuu, ikiwamo ugomvi wa nchini Rwanda na Burundi, zaidi mauaji ya kimbari,” anasema Mzee Mwinyi.

Anasema kwa kipindi cha miezi mitatu cha mauaji hayo, kuanzia Aprili hadi Julai, mwaka 1994, hawezi kukisahau na kuamua kuitisha mkutano ulioshirikisha serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais wa Rwanda, Juvenal Habyarimana pamoja na Cyprien Ntaryamira rais wa Burundi, wakati huo.

“Marais hawa wawili kila mmoja alikuja (Dar es Salaam) na ndege yake. Rais Habyarimana alikuwa amempa lifti balozi wetu katika nchi yake, Saleh Tambwe (kuja Tanzania). Walipokuwa wanarejea makwao, Rais Habyarimana ambaye ndege yake ilikuwa na kasi kubwa zaidi, aliamua kumpa lifti Rais wa Burundi, Ntaryamira…ndege iliyowawabeba marais hao ilitunguliwa.”

Wote waliokuwamo kwenye ndege hiyo wakafa…ikazuka vita mara moja nchini humo na kufumba na kufumbua, Watanzania karibu 2,000 wakaenda ubalozini kuomba msaada wa dharura wa ulinzi na kurejeshwa Tanzania.”

Mzee Mwinyi anaeleza namna alivyoshtushwa na vifo vya marais hao, kwa kuwa duniani tukio la viongozi wawili wa nchi kufa kwenye tukio moja, huwa ni nadra.

“La kusikitisha zaidi ni kwamba marais wote wawili walikuwa nchini mwetu, kutafuta suluhu na kukomesha mauaji yaliyokuwa yanaendelea katika nchi zao, kuleta amani, maelewano na ushirikiano...kilichokuwa kibaya zaidi...kifo cha Rais Habyarimana kuwa chanzo cha mauaji ya kimbari,” Mzee Mwinyi anasimulia kwenye kitabu chake.

Mzee Mwinyi anasema kamati ya Umoja wa Mataifa iliyoanzishwa na kutoa taarifa yake Desemba 9, mwaka 1994, ilikadiria kwamba raia 500,000 waliuawa, ingawa uchunguzi uliofanywa na serikali ya Rwanda ulisema idadi ya vifo ilifikia watu 951,018.

Anasema historia ya Rwanda na Burundi, inabakia kuwa somo la kujifunza madhara ya ubaya wa ubaguzi wa kikabila, na kwamba ukoloni ulichangia kuandaa mazingira ya kushindwa kujitawala kwa amani na kuendelea.

“Tufanye kila tuwezalo kuua kabisa mbegu za ukabila zilizosalia na kujenga uchumi wa nchi zetu, kwa kuzingatia maslahi ya watu wetu, nchi zetu na bara letu,” anasema Mzee Mwinyi.

KIKWAZO CHA KIHISTORIA

Hata hivyo, hilo si suala geni. Ikirejewa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, katika kitabu chake cha 'Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu', anakiri kadhia hiyo imo katika yaliyoupa ugumu uongozi wa nchi.

Mwinyi analitaja suala hilo kuirithi nchi tangu zama za mtangulizi wake, Mwalimu Julius Nyerere, aliyetoka nalo mwaka 1980, naye (Mwinyi) akilikuta lina miaka mitano.

"Ili kukabiliana na kushuka kwa uzalishaji na tija kwenye sekta ya umma, kwenye sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi mwaka 1980, CCM ilitangaza sera mpya ya tija na kusema kuwa sasa wafanyakazi watalipwa kulingana na matokeo.

"Kwa maana hiyo, iwapo kiwanda cha umma kitapata hasara, menejimenti na wafanyakazi hawatakuwa na haki ya kulipwa nyongeza ya mshahara au kupandishwa vyeo, lakini bonasi zitalipwa pale ambapo kiwanda kimeongeza uzalishaji, tija na faida," Mwinyi anasema.

Katika kitabu chake hicho kilichozinduliwa na Rais Samia mwezi huu, Mwinyi anabainisha kuwa ili kutekeleza maagizo hayo ya CCM, serikali ilitoa Waraka wa Serikali Na. 1 wa Mwaka 1981 na kisha ikatunga Sheria ya Baraza la Tija la Taifa.

     

Join our Newsletter