Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 583993

Siasa of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

NCCR-Mageuzi kwenda mahakamani kupinga Ndugai kujiuzulu

NCCR-Mageuzi kwenda mahakamani kupinga Ndugai kujiuzulu NCCR-Mageuzi kwenda mahakamani kupinga Ndugai kujiuzulu

Chama Cha NCCR-Mageuzi kimesema kinakusudia kwenda mahakamani kupinga iwapo kutakuwa na mchakato wowote wa kumpata Spika mpya wa Bunge la Tanzania ili kulinda uhai wa Katiba ya nchi.

Chama hicho kimesema wanachukua uamuzi huo baada ya kubaini utaratibu aliotumia aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kujiuzulu ni batili na unaenda kinyume na matakwa ya katiba inayotumika kwa sasa.

Jana Alhamisi Januari 6, 2022 aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai alitoa taarifa kwa umma kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuzulu nafasi hiyo.

Muda mfupi baada ya taarifa ya Ndugai, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo alithibitisha kupokea barua ya Ndugai ikimtaarifu kujiuzulu nafasi hiyo.

Akizunumza leo Ijumaa Januari 07, 2022 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amedai kuwa utaratibu aliotumia Ndugai hauko sahihi na kwa sasa viongozi wa chama hicho wanashauriana na wanasheria wao kabla ya kwenda kuiomba mahakama kuingilia kati uvunjifu huo wa Katiba.

“Tunakusudia kwenda mahakamani kuomba utaratibu huu ambao umekiukwa na nibatili. Na tukiruhusu hivi ujuhe watoto wetu wanaosoma leo rejea Tanzania itakayoonekana miaka ijayo itakuwa kichekesho Duniani,

Advertisement “Yaliyofanyika na utaratibu wote uliotumika jana hekima haikutumika na busara inakataa, kikatiba, kisheria, kimantiki na kiutamaduni tu inakataa,” amesema Mbatia

Amesema  licha ya kwamba Ndugai alipata fursa ya kushika nafasi hiyo kwa kudhaminiwa na chama lakini wanapaswa kutambua alipigiwa kura na wabunge wote hivyo alitakiwa  kwenda kujiuzulu kwenye vikao vya bunge na si kuandika barua kwenda kwa Katibu wa Chama chake.

“Lakini kwa kufanya vile Ndugai amekiuka hata kiapo chake kwa sababu kama mbunge alisimama kwamba atahifadhi na kuitetea Katiba ya nchi na kuwa mtiifu na baadae ametoka hadharani unaenda kuiomba radhi Serikali na inaonesha hata hivi viapo havina maana,”amesema

Amesema  kwa kuwa utaratibu aliotumia ni batili bado wanamtambua Ndugai ni Spika na utaratibu wowote utakaoendelea kama katiba haitafuata ni mgogoro mkubwa na hiyo inadhihirisha madhila yote yanayojitokeza kuna uhitaji wa Katiba mpya inayotokana na maoni ya watanzania.

“Ndio maana tunasema Katiba inayotumika kwa sasa ina migogoro mingi ndiyo maana kila mtu anaamua kujifanyia anachotaka na tukiendelea kuruhusu haya ikiwemo migongano inayoendelea isiposimamiwa vizuri taifa letu litaangamia,” amesema Mbatia

Amesema watatumia ibara ya 108 kifungu kidogo cha pili pamoja na ibara ya 26 kwa maslahi ya taifa na dunia inayomtaka kila mtu kuifuata na kuitii katiba ya nchi na sheria na utaratibu wake uliowekwa.