Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541408

Siasa of Monday, 7 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

NCCR yaona matumaini kwa Samia

Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, akizungumza jana katika makao makuu ya chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam, alisema wamekuja na hoja hizo nne ili kukuza mtazamo wa pamoja katika taifa kuhusiana na masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Alisema mahitaji makuu ya Rais Samia ni kulinda utu katika mazingira yanayomzunguka pia mifumo inayozingatia afya na elimu bora, inayowezesha kutambua na kutumia utajiri uliomo nchini, ili kutengeneza fursa.

Kuhusu uchumi, alisema usalama wa uhai wa wanajamii unategemea hali ya uchumi wa jamii husika, hivyo mfumo uliopo unategemea mzunguko wa fedha ambao kwa sasa ni mdogo hivyo kuwaweka watanzania shakani.

“Rai yetu kwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wawe na utashi wa kupitia bajeti itakayozingatia kwamba kipaumbele namba moja ni usalama na uhai wa kila mtanzania, bajeti iwe ya kutuunganisha na kwa kupunguza tofauti zetu kwenye mahitaji muhimu ya misingi ya mwanadamu.”