Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585580

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Nape awajulia hali waandishi walionusurika ajalini

Nape awajulia hali waandishi walionusurika ajalini Nape awajulia hali waandishi walionusurika ajalini

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amewajulia hali majeruhi wa ajali iliyotokea juzi katika Wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu.

Waziri Nape alisema kuwa amefarijika kuona majeruhi wanaendelea vizuri mara baada ya kupata matibabu na hata sasa angalau wanaweza kuzungumza kidogo, majeruhi hao ni Tunu Herman na Vanny Charles ambao ni wanahabari.

"Nawapongeza madaktari wa hospitali ya Bugando na watumishi wote wa afya kwa kutoa matibabu mazuri kwa majeruhi hata sasa kama tulivyowaona angalau wanajitambua, pia nashukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa jitihada mbalimbali walizofanya ili kusaidia majeruhi hawa waweze kupata msaada wa haraka" alisema Waziri Nape