Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551467

Habari za Afya of Friday, 13 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Nchi za SADC zatakiwa kujiimarisha kutengeneza chanjo

Nchi za SADC zatakiwa kujiimarisha kutengeneza chanjo Nchi za SADC zatakiwa kujiimarisha kutengeneza chanjo

JUMUIYA ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC imetakiwa kuimarisha uwezo wa ndani wa kutengeneza chanjo na dawa ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa dawa na chanjo panapotokea majanga na magonjwa ya milipuko inayosababisha vifo vingi katika Bara la Afrika.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC Dk. Stergomena Tax wakati akitoa taarifa ya utendaji ya Jumuiya hiyo katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC na kuongeza kuwa janga la UVIKO -19 limekuwa na changamoto kubwa husasani katika upatikanaji wa chanjo kwa wananchi wote wa Jumuiya hiyo.

Dk Tax ambaye ameitumia fursa hiyo kuwaaga Mawaziri wa SADC kutokana na kumaliza muda wake amezisihi nchi za Afrika kuweka nguvu za pamoja katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 na kuziomba nchi,taasisi na Jumuiya za Kimataifa kuridhia nchi masikini ziwezo kutumia teknolojia zao katika kuzalisha dawa na chanjo ili huduma hiyo ipatikane kwa wananchi wote.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ambaye ameongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi amezitaja baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa katika Mkutano huo kuwa ni pamoja na kumchagua mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba, kwa upande wake amesema Tanzania imeendelea kuwa mfano katika kufuata sheria na taratibu za Jumuiya mbalimbali ambazo Tanzania ni mwanachama ikiwa ni pamoja na ulipaji wa ada kwa wakati.

Mkutano huu wa siku mbili wa Baraza la Mawaziri wa SADC ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17 na Agosti 18, 2021 Lilongwe nchini Malawi na Tanzania itawakilishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu, ambapo pamoja na mambo mengine utaidhinisha nyaraka mbalimbali za kisheria ikiwemo itifaki ya takwimu.