Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 14Article 551518

Siasa of Saturday, 14 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Ndugai Afafanua "Hakuna ulazima Wabunge kuchanja"

Ndugai Afafanua Ndugai Afafanua "Hakuna ulazima Wabunge kuchanja"

Ofisi ya Bunge, imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji zinazosambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinazodai wabunge ambao hawatachanja chanjo ya Covid 19 hawataruhusiwa kuingia bungeni.

Taarifa iliyotolewa leo na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge inaeleza taarifa ambazo zinasambaa katika baadhi ya mitandao hazina ukweli na kwamba maelekezo ambayo Spika Job Ndugai ameyatoa ni kuwasisitiza wabunge kujitokeza kwa hiyari kuchanjwa chanyo hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa Ofisi ya Bunge imeandaa utaratibu utakaowezesha wabunge wote kupata chanjo hiyo katika viwanja vya bunge huku ikiwasisitiza wabunge kujitokeza kwa hiyari ili kupata chanjo kwa ajili ya kujikinga wao na wengine.