Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541504

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ndumbaro: Ruksa kufuga nyuki hifadhini    

Ndumbaro: Ruksa kufuga nyuki hifadhini       Ndumbaro: Ruksa kufuga nyuki hifadhini    

WAZIRI wa Maliasiali na utalii Dk Damas Ndumbaro amewaruhusu wafugaji wa nyuki kuendelea kufanya shughuli zao kwenye hifadhi ya taifa ya Kigosi iliyopo wilayani Bukombe mkoani Geita lakini serikali itatoa muongozo jinsi ya kufanya shughuli hizo kwa utaratibu.

Dk Ndumbaro alitoa maelekezo hayo alipokutana na umoja wa wafuga nyuki wilayani humo na kutolea ufafanuzi tamuko alilolitoa hivi karibuni juu ya kusitishwa shughuli zote za kibinadamu katika hifadhi zote za taifa ikiwemo hifadhi ya taifa ya kigosi.

Aidha Dk.Ndumbaro ameruhusu shughuli za ulimaji wa asali kwenye hifadhi hiyo kuendelea kama kawaida tofauti na tamuko alilolitoa mwezi mei mwaka huu lililokuwa likiwataka wafugaji wa nyuki kutumia siku 30 pekee kulima asali kwenye hifadhi hiyo badala ya siku 60.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wafuga Nyuki wilaya ya Bukombe, Emmanuel Maganga alisema kauli hiyo imewapa matumaini kwani shughuli hizo zimekuwa na mchango mkubwa kwenye pato la tafa na hivyo muongozo uliotolewa na waziri utaongeza chachu ya uzalishaji wa asali.

Maganga alisema umoja wao una vikundi 30 vya wafuga nyuki, vyenye jumla ya wafuga nyuki 1177, na wasaidizi 11770, ambao wamekuwa wakichangia kwenye pato la taifa takribani Sh milioni 76.3 kila mwaka kutokana na kulipa tozo ya Sh5600 kwa kila mmoja.

Katibu wa wafuga nyuki Bukombe, Charles Makaya alisema wilaya hiyo imefanikiwa kuvuna na kusafirisha ndani na nje ya nchi takribani kilo milioni 2.3 za asali sawa na tani 2,331.2 pamoja na kilo za nta 177,466 sawa na tani 177.466 kwa miaka minne kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2020/2021.

Join our Newsletter