Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 04Article 545218

Habari Kuu of Sunday, 4 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ndumbaro 'awapa tano' TATO

Ndumbaro 'awapa tano' TATO Ndumbaro 'awapa tano' TATO

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema anaunda Kamati ya Ushauri ya masula ya Utalii ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikumba sekta hiyo.

Amesema wakati wa mazungumzo na Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Wasafirishaji Watalii (TATO) nakuahidi kutoa nafasi tatu za uwakilishi katika kamati hiyo.

"Ninapokuwa na suala nyeti la Utalii nimekuwa nikiwashirikisha TATO kutokana na jinsi umakini wao na kujitoa kwao katika suala la utalii" alilisitiza Dkt.Ndumbaro

Amesema licha ya kuwa katika sekta yaUtalii kuna vyama vya Utalii zaidi ya kumi lakini TATO imekuwa namba moja katika kutafuta suluhu za changamoto badala ya kuwa Walalamikaji kama vyamr vingine vilivyo.

Mwenyekiti wa TATO, Willybroad Chamburo amemhakikishia Waziri Dkt. Ndumbaro kuwa katika Uongozi wake wataendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa ajili aya maslahi mapana ya Sekta ya Utalii.