Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553600

Habari Kuu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Ni aibu kuona Askari anachukua rushwa"- Rais Samia

Askari Polisi waonywa kuhusu vitendo vya rushwa Askari Polisi waonywa kuhusu vitendo vya rushwa

Rais Samia, amekemea vitendo vya rushwsa vinavyofanywa na baadhi ya Polisi hasa wa barabani katika maeneno yao kazi.

Rais Samia Ametoa kauli hii wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Jeshhi la polisi kilichofunguliwa hii leo,nakuwataka Askari wote kuzingatia maadili yao ya kazi kwani vitendo hivyo vinalishushia hadhi jeshi hilo.

"Ni aibu kuona kwenye simu zetu askari aki negotiate rushwa, hasa askari wa barabarani, vi clip vinarushwa tu askari anachukua rushwa, hawajajua teknolojia, mtu anamrekodi kwa kalamu, askari anaelekeza kabisa huku akichukua burungutu lake". - Rais Samia

Amepinga hoja zinazotumiwa kuhalalisha rushwa kwa kigezo cha njaa na kusema kuwa haina mashiko kwani wenngi wanao fanya vitendo hivyo hawana maadili ya kutosha, amewasisitiza askari wote kuzingatia weledi na maadili ya kazi ili kuondoa vitendo hivyo vinavyolilettea jeshi hilo aibu.