Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541534

Habari Kuu of Monday, 7 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Nyumba za kisasa za Polisi DSM "zianze kutumika"; (+video)

Nyumba za kisasa za Polisi DSM Nyumba za kisasa za Polisi DSM "zianze kutumika"; (+video)

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, imetembelea na kukagua mradi wa nyumba za Makazi ya Askari na baadae ikatoa mapendekezo kwa Serikali kuona namna bora ya nyumba hizo kuweza kutumiwa na Jeshi la Polisi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamisi Chilo amesema kamati imependekeza na kushauri kuanza kutumika kwa nyumba za Polisi zilizopo Kunduchi, Mikocheni na Oysterbay ambapo nyumba hizo zitasaidia kupunguza changamoto za makazi kwa askari wa Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa, ziara ya kamati hiyo imetoa mwanga kwa Jeshi hilo na kwamba yeye na watendaji wake wamejipanga na kwamba wanasubiri kuruhusiwa ili askari Polisi waweze kuzitumia nyumba hizo.