Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552253

Dini of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Padre Paul Haule wa St Peter's afariki dunia

Aliyekuwa Paroko Msaidizi , Padre Paul Haule Aliyekuwa Paroko Msaidizi , Padre Paul Haule

HABARI zilizotufikia ni kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Petro ‘St Peters’ jijini Dar es Salaam, Paul Haule, amefariki dunia leo saa 10:30 jioni wakati akitibiwa katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa iliyopo Ukonga.

Taarifa za awali zinasema mwili wa Padre Haule ambaye alikua amelazwa kwa siku kadhaa umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Mbali na kuwa paroko msaidizi, Padre Haule alikuwa mkurugenzi wa matangazo Radio Tumaini.