Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 05Article 541153

Habari Kuu ya

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Panya Magawa Mtegua Mabomu Astaafu

Panya Magawa Mtegua Mabomu Astaafu Panya Magawa Mtegua Mabomu Astaafu

PANYA dume kutoka Tanzania, maarufu kwa jina la Magawa ambaye mwaka jana alitunukiwa nishani ya kimataifa ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini Cambodia, anastaafu kazi mwezi huu wa Juni 2021.

Magawa alizaliwa Tanzania, Novemba 5, 2014 akiwa na uzani wa KG 1.2 na urefu wa Sentimita 70, alipewa mafunzo na Shirika lisilo la Kiserikali la Apopo kutoka Ubelgiji lenye makao yake Morogoro Tanzania na alipewa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini.

Wasimamizi wake wanasema Magawa mwenye umri wa miaka saba kwa sasa ameanza kupunguza kasi yake ya kutegua mabomu kwa kuwa amezeeka na ni wakati wake wa kupumzika.

Shirika la Matibabu ya Wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA lilimtunza medali ya dhahabu kwa kujitolea kwake kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia.

Shirika hilo limekuwa likiwalea wanyama wanaofahamika kama – PanyaShujaa- kugundua uwepo wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu miaka ya 1990. Inadhaniwa huenda kuna hadi mabomu milioni sita ya kutegwa ardhini katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Bara Asia.

Japo ni mkubwa kuliko aina nyingine za panya, Magawa ni mdogo ni mwepesi kiasi kwamba hawezi kulipua mabomu akitembea juu.

Panya hao wanafundishwa kubaini kemikali iliyotumiwa katika vilipuzi, kumaanisha wanaweza kupuuza vyma vikuukuu na kutafuta mabomu kwa haraka zaidi. Wanapopata kilipuzi wanakuna juu yake na kuwaonesha binadamu wafanyakazi wenzao.

Magawa ana uwezo wa kusaka mabomu katika eneo lenye ukubwa wa uwanja wa mpira wa tennis kwa muda wa dakika 20 jambo ambalo Apopo linasema itamchukua mtu aliye na kifaa cha kubaini vifaa vya chuma kati ya siku moja hadi nne.

Panya huyo anafanya kazi kwa saa moja na nusu kwa siku nyakati za asubuhi na anakaribia kustaafu, lakini mkurugenzi mkuu wa PDSA Jan McLoughlin amesema kazi yake katika shirika la Apopo ilikuwa “ya kipekee na ya kuridhisha”.

Join our Newsletter