Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541423

xxxxxxxxxxx of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Pasipoti kielektroniki zapunguza utapeli

IDARA ya Uhamiaji katika Wizara ya Mambo ya Ndai ya Nchi imesema huduma za kupata hati za kusafiria kwa njia ya mtandao zimepunguza utapeli katika kuzipata.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala aliyasema hayo baada ya kuwepo mijadala katika mitandao ya kijamii kuhusu hatua za kuwasimamisha kazi askari wa idara hiyo kwa kutoa adhabu isivyo kawaida kwa raia aliyedaiwa kuhusika kutapeli wananchi.

Ilidaiwa katika mijadala hiyo kuwa, baadhi ya wafanyakazi wa Uhamiaji hushirikiana na matapeli kuwarubuni watu wanaofika katika ofisi zao kutafuta pasipoti kwa kuwatoza fedha ili wazipate kwa haraka.

Alisema kwa simu kuwa hivi sasa hakuna matukio hayo kwa wingi hasa baada ya kuanza utaratibu wa kutoa pasipoti za kusafiria kielektroniki.

“Hakuna kitu kama hicho kwa sasa. Huduma za uhamiaji mara nyingi zamani walikuwa wanatumia ‘middle man’ (mtu wa katikati) au vishoka, sasa mtandao unakataza watu wa kati, tunamuhoji yeye mwenyewe mhusika.”

“Kwa njia hiyo, tumepambana sana na tabia hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Dk Makakala alipozungumza na HabariLEO.

Hivi karibuni ilisambaa video mitandaoni ikimuonesha askari wa Uhamiaji wakitumia nguvu dhidi ya mtuhumiwa wa utapeli, Alex Kyai.

Dk Makakala alilaani kitendo hicho na askari hao walisimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

“Mara nyingi sana watu walikuwa akijitambulisha kama maofisa uhamiaji, wametuchafua sana na kwa kiwango kikubwa tumedhibiti, kitendo walichofanya juzi haikutakiwa kutumia nguvu ile,” alisema.

Alisema mashauri dhidi ya askari hao yanaendelea na hatua zaidi zikichukuliwa huku akiahidi kwamba umma utajulishwa.

Alisema pia mtuhumiwa amekabidhiwa kwa vyombo husika vya sheria.

Huduma za pasipoti kwa njia ya mtandao zilianza kutolewa mwaka 2018 baada ya kuzinduliwa na Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli Februari mwaka huo.

Join our Newsletter