Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541807

Habari za Afya of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

‘Pelekeni hospitali watoto wenye mguu kifundo’

‘Pelekeni hospitali watoto wenye mguu kifundo’ ‘Pelekeni hospitali watoto wenye mguu kifundo’

Kitengo cha Tiba ya Mazoezi ya Viungo katika Hospitali ya Wilaya ya Sengerema kimetoa mwito kwa wazazi na walezi wa watoto wenye tatizo la mguu kifundo, kupeleka watoto hao kwa ajili ya matibabu kwa kuwa ni tatizo linalokwisha.

Kiongozi Mkuu wa Kitengo cha Tiba ya Mazoezi ya Viungo katika hospitali hiyo, Dk Charles Gabriel, alisema katika mazungumzo na HabariLEO kuwa, tatizo la mguu kifundo linatokana na changamoto ya mtoto wakati wa ukuaji.

Aliwataka wazazi na walezi hao kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanapeleka watoto hospitalini kwa matibabu kwa kuwa tatizo hilo linatibiwa katika hospitali mbalimbali nchini zikiwemo hospitali ya rufaa za SekouToure, Geita, Hospitali ya Wilaya Sengerema na Shirati mkoani Mara.

Alisema katika Mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Ukerewe inaongoza kwa watoto wengi wenye tatizo hilo.

“Huduma hizi zinachukua wiki 12 na mtoto anafungwa ‘POP’ na kufanyiwa operesheni ndogo, kisha anatumia viatu maalumu kwa muda wa miaka minne,”alisema.

Dk Charles alisema hospitali yao kwa kushirikiana na Shirika la Tanzania Footcare (TCCO) wataendelea kutoa elimu ili kuongeza uelewa katika jamii juu ya tatizo hilo.

Mkazi wa Wilaya ya Ukerewe, Meshack Monja, alisema watoto wake wana tatizo hilo na yeye alikuwa akitumia dawa za kienyeji, lakini hawaponi akaamua kuwapeleka watoto hospitalini.

Join our Newsletter