Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553651

Habari Kuu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: millardayo.com

Picha12:Kutoka eneo lililokuwa na majibizano ya Risasi DSM

Picha12:Kutoka eneo lililokuwa na majibizano ya Risasi DSM Picha12:Kutoka eneo lililokuwa na majibizano ya Risasi DSM

NI Agosti 25, 2021 ambapo Polisi wamefanikiwa kumdhibiti Mtu mmoja ambae alikua anafyetua ovyo risasi hewani karibu na Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi limesema idadi ya Watu waliouwawa na Mtu mwenye Bunduki aliekua akifyetua risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa Dar es salaam ni Watu wanne huku kati yao Watatu wakiwa ni Polisi na mmoja ni Mlinzi wa Kampuni binafsi ya ulinzi.

“Leo August 25 2021 tumekutwa na tukio baya kabisa, tukio la kihalifu ambalo limepoteza maisha ya Watu wanne na watatu kati yao ni Askari Polisi, limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni Askari wetu walikua kazini akatokea Mtu akawashambulia kwa Bastola na alipowashambulia na kuanguka alichukua Bunduki za Askari hao na kuanza kurusha risasi ovyo kuelekea Ubalozi wa Ufaransa”- Jeshi la Polisi

Millardayo.com imekuwekea picha 12 kutoka katika eneo hilo la tukio.

..........