Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585565

Uhalifu & Adhabu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Polisi Iringa wakamata KG.65 za meno ya tembo

Polisi Iringa wakamata KG.65 za meno ya tembo Polisi Iringa wakamata KG.65 za meno ya tembo

Jeshi la Polisi mkoani Iringa kwa kushirikiana na Hifadhi ya taifa ya Ruaha limekamata meno ya tembo yenye uzito wa kilogram 65 yanayokadiriwa kuwa na gharama ya Zaidi ya shilingi milioni miambili hali inayoashiria kurejea kwa vitendo vya ujangili katika hifadhi.

Akitoa taarifa juu ya matukio mbalimbali ya uhalifu kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Kamishina Msaidizi wa Polisi Allan Bukumbi amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao waliokuwa wakisafirisha nyara hizo za serikali kunatokana na opparesheni zinazofanywa jeshi hilo.