Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573427

Siasa of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Polisi kuchunguza kifo kigogo wa CHADEMA

Polisi kuchunguza kifo kigogo wa CHADEMA Polisi kuchunguza kifo kigogo wa CHADEMA

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la kifo cha Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Buswelu mkoani Mwanza, Erasto Makaranga.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Ramadhani Ng'anzi amesema maofisa wa jeshi hilo tayari wamefika katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure kwa ajili ya uchunguzi wakina wa mwili wa kiongozi huyo.

"Bado askari wetu wako kwenye eneo la tukio wakiwa wanakusanya ushahidi kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwa hiyo tusubiri wamalize uchunguzi wao na tukikamilisha tutatoa taarifa," amesema Ng'anzi

Awali, akizungumza kwa njia simu Msemaji wa familia hiyo, Benjamini Makaranga amesema familia iliapanga kufanya maziko ya mpendwa wao leo Jumatatu Novemba 22,2021 lakini juhudi za kukamilisha mazishi hayo zimegonga mwamba baada ya maofisa wa jeshi la polisi kufika na kuzuia mwili huo kuchukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

"Tumewasili leo asubuhi katika chumba cha hospitali ya rufani ya Sekou Toure kwa ajili ya kuchukua mwili lakini tumezuiwa na watu wa usalama wakidai wanataka kwanza uchunguzi wa mwili ufanyike ndiyo turuhusiwe kuzika," amesema Benjamini

Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Macrina Makaranga baada ya familia kubaini kutoweka kwa ndugu yao juhudi za kutoa taarifa katika vituo vya polisi zilifanyika bila mafanikio ndipo walipoamua kutafuta mwili wake katika hospitali ya rufaa ya Kanda ya Bugando na hospitali ya rufani ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure ndipo walipoukuta ukiwa na majeraha kichwani.

"Tulimtafuta Bugando hatukumpata baadae tukaenda Sekou Toure mara tatu hatukumpata baadae tuliporudi mara ya nne ndiyo tukaukuta mwili wake ukiwa unaonekana una majeraha katika sehemu ya kichwani na mkono wake unaonekana kama umevunjika," amesema Macrina

Erasto Makaranga anadaiwa kutoweka nyumbani kwake Novemba 17 mwaka huu na mwili wake kupatikana Jumamosi Novemba 21,2021 ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufani ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure.