Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 23Article 553123

Habari za Mikoani of Monday, 23 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Polisi wachunguza ajali iliyoua watano Songwe

Wanaume watahadharishwa kunyonya maziwa ya wake zao Wanaume watahadharishwa kunyonya maziwa ya wake zao

POLISI Mkoani Songwe inachunguza chanzo cha ajali iliyotokea alfajiri ya Agosti 23 nakusababisha vifo vya wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe, ACP Janeth Magomi amesema polisi wameanza uchunguzi wa ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Hanseketwa- Old Vwawa Wilayani Mbozi.

Amesema waliofariki ni wafanyakazi wanne wa TRA Mkoa wa Mbeya na Mwingine anayefanya kazi TRA – Tunduma.

“Wate walikua wakitekeleza majukumu yao ya doria mipakani ambapo walishuku gari moja kuwa inaweza kuwa ikisafirisha magendo,” alisema.

Hadi sasa TRA haijatoa tamko lolote kuhusiana na ajali hiyo. Mashuhuda wa ajali hiyo wamenyoshea kidole mwendokasi na kukosa umakini wa madreva kama chanzo cha ajali hiyo.