Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 27Article 554065

Habari Kuu of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Polisi waliouwawa na Muhalifu Salenda kuagwa leo

Askari Polisi  waliouwawa na Muhalifu Salenda kuagwa leo Askari Polisi waliouwawa na Muhalifu Salenda kuagwa leo

Askari waliouwawa katika tukio la uhalifu lililotokea Agosti, 25,2021 inatarajiwa kuagwa leo katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lilozua taharuki kubwa jijini humo, mara baada ya muhalifu haliyefahamika kwa majina ya Hamza Mohamed,kuwashambulia Polisi na kupelekea vifo vya askari 3 na mlinzi mmoja wa kampuni ya SGA, huku Polisi wakifanikiwa kumdhibiti kwa kumuua Muhalifu huyo.

Bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo, huku tayari familia ya Muhalifu ikiwa Polisi kwa ajili ya mahojiano.