Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 12Article 542332

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 12 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Polisi yakamata wezi wanaotumia pikipiki

Polisi yakamata wezi wanaotumia pikipiki Polisi yakamata wezi wanaotumia pikipiki

Jeshi la Polisi Kanda Kaalum ya Dar es salaam linawashikilia Watuhumiwa wa vitendo vya kihalifu ambao ni kero kwa Wananchi wa Dar es salaam.

Katika oparesheni hiyo kali inayoendelea Polisi wamemkamata Edson Boniface (24), mkazi wa Kimara na wenzake 09 ambao wamekuwa wakitumia pikipiki (boxer ) kupita mitaani na maeneo yenye miamala ya pesa na kupora kwenye ofisi hizo au kuvizia wanaochukua pesa na kuwafuatilia nyuma hatimaye kuwapora.

“Katika idadi ya wahalifu hao wengine wamekuwa wakipokea mali za wizi, kuiba vifaa vya ujenzi kwenye miradi mbalimbali, majina yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi, Watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na gari moja aina ya Toyota Canter yenye namba za usajili T.134 DST ikiwa na nondo tani moja”

“Watuhumiwa wengine walikamatwa na mali za wizi na simu za mkononi 118 zilizoporwa katikati ya jiji, Kompyuta mpakato (Laptop) 29, kompyuta 02 kwa ajili kufuta kumbukumbu(flash), Tv 13 na vifaa mbalimbali vya magari” ———Kamanda Muliro

MKE WA TB JOSHUA AFICHUA MWANZO MWISHO ALIVYOFARIKI, ALIOGA, IBADANI, AKAFIA CHUMBA MAALUM