Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 14Article 542476

Siasa of Monday, 14 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Profesa Baregu afariki

Profesa Baregu afariki Profesa Baregu afariki

Mwanachama wa CHADEMA na mwanazuoni, Prof. Mwesiga Baregu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha  amesema, “amefariki saa tano usiku wa kuamkia leo akiwa ICU (chumba cha uangalizi maalum)  na alikuwa hapo kwa takribani siku 15.”

Mkurugenzi wa Itikadi na Uhusiano wa kimataifa wa Chadema, John Mrema amesema chama kitatoa taarifa rasmi taarifa baada ya kikao na wanafamilia.

“Tunaelekea hospitali ya Muhimbili kukutana na wanafamilia halafu tutatoa taarifa rasmi,” Mrema.

BREAKING: MTANGAZAJI FREDWAA AFARIKI