Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541267

Habari za Mikoani ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAS mpya Moro azungumzia asilimia 100 ya makusanyo

RAS mpya Moro azungumzia asilimia 100 ya makusanyo RAS mpya Moro azungumzia asilimia 100 ya makusanyo

WAKURUGENZI wa halmashauri za Mkoa wa Morogoro, wametakiwa kufikisha asilimia 100 ya makusanyo ya mapato ya ndani katika maeneo yao kabla ya mwaka kumalizika kwa mwaka fedha wa serikali wa Juni 30 ,2021.

Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Mariam Mtunguja, alitoa agizo hilo jana kwa wakurugenzi wa halmashauri tisa wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa, Emmanuel Kalobelo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima (kushoto) akikabidhi Mwenge wa Uhuru 2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai kijijini Chekereni Wilaya ya Same juzi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa).

‘’Tunaelekea tarehe 30 ya mwezi wa sita, naamimi kila Mkurugenzi wa halmashauri amejiwekea asilimia za ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yake, hivyo naomba mkasimamie zoezi hili kikamilifu ili tuepuke kupata hati chafu katika mkoa wetu, Mkaguzi wa ndani naye ahakikishe anafuatilia hili”alisema Mtunguja.

Katibu tawala aliwataka watumishi wa umma kumpa ushirikiano wa dhati katika kutekeleza majukumu yake kuyafikia malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali katika kufikia uchumi wa kati wa kiwango cha juu.

Alitumia fursa hiyo kusisitiza juu ya ushirikiano na kuheshimiana miongoni mwa watumishi katika kufanya kazi zao ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi yenye tija kwa mkoa huo na Taifa.

Aliyekuwa Katibu Tawala, Kalobelo , aliwaomba wafanyakazi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa na watumishi wote wa umma mkoani humo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mtunguja kama walivyompa yeye kufikisha mkoa katika malengo yaliyokusudiwa.

Join our Newsletter