Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 12Article 546748

Habari za Mikoani of Monday, 12 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

RC Hapi aanza kufukua ya Mkurugenzi wa Serengeti

RC Hapi aanza kufukua ya Mkurugenzi wa Serengeti RC Hapi aanza kufukua ya Mkurugenzi wa Serengeti

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi ameweka bayana kuwa ataanza kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Serengeti, Juma Hamsini ili kukomesha urasimu unaofanywa na baadhi ya viongozi dhidi ya wawekezaji na hivyo kuchelewesha maendeleo katika Mkoa huo.

RC Hapi amesema hayo leo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Robert Gabriel ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Amedai kuwa Hamsini amekwamisha ujenzi wa uwanja wa ndege Burunga wilayani humo, ambapo Hifadhi ya TANAPA ilijitolea Sh bilioni 1.2 na baadhi ya wafanyabiashara walijitolea kugharamia mafuta ambayo yangetumiwa kwenye magari ya kufanya kazi mbalimbali katika ujenzi huo.

Amesema licha ya mradi huo kuzinduliwa na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete mpaka sasa hakuna hatua hata moja iliyotekelezwa kutokana na "danadana" za Mkurugenzi huyo ambaye ilifika wakati akaanza kuwataka TANAPA wapeleke fedha walizoahidi kwenye Halmashauri.

Katika tukio la kukabidhi ofisi Mhandisi Gabriel ambaye awali alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara alisema, “Kazi yangu ilikuwa nyepesi kwasababu Mungu alitangulia, Mungu akitangulia mwanadamu ananufaika,” amesema Mhandisi Gabriel.

Naye Hapi amepokea ushauri huo na kuwataka viongozi wote kukaa mkao wa kuchapa kazi kwasababu amedhamiria kukidhi matarajio ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuleta mapinduzi ya kimaendeleo mkoani humo.