Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 12Article 542326

Habari za Mikoani of Saturday, 12 June 2021

Chanzo: millardayo.com

RC Homera amsimamisha kazi Mtunza hazina (+video)

RC Homera amsimamisha kazi Mtunza hazina (+video) play videoRC Homera amsimamisha kazi Mtunza hazina (+video)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amemsimamisha kazi Mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Edward Andendekisye na kuagiza Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani watumishi saba wa halmashauri hiyo kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh. milioni 400.

“Watendaji hawa wanapaswa kusimamishwa kazi na kukaa mahabusu hadi pale watakapolipa fedha wanazodaiwa ambazo pia zimetajwa kuwa chanzo cha halmashauri hii kupata hati isiyoridhisha,” Homera.