Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 15Article 542869

Habari za Mikoani of Tuesday, 15 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

RC Kunenge aagiza ukusanyaji mapato ufuate sheria

RC Kunenge aagiza ukusanyaji mapato ufuate sheria RC Kunenge aagiza ukusanyaji mapato ufuate sheria

Kunenge ametoa agizo hilo aliposhiriki katika baraza maalumu la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya hiyoi kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2019/2020. Amesema ni vema vyanzo vikahakikiwa ili kuweka mikakati ya kuongeza mapato.

Aidha ameitaka Halmashauri hiyo kuangalia maeneo mengine ya vyanzo vipya vya mapato na siyo kuongeza viwango vya kodi itakayoleta kero kwa wananchi.

Kunenge pia amesema kuanzia sasa atakayehusika kujibu hoja za CAG ambazo hazijafungwa ni yule aliyezalisha katika eneo laje na si Mkurugenzi, lakini pia maeneo yaliyoonekana kuwa na ubadhilifu iwekwe mikakati ya kuondoa shida iliyopo.