Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541768

Habari za Mikoani of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

RC Makalla Aingilia Kati Mgogoro wa Mwanaume Aliyemtapeli Mpenzi Wake

RC Makalla Aingilia Kati Mgogoro wa Mwanaume Aliyemtapeli Mpenzi Wake RC Makalla Aingilia Kati Mgogoro wa Mwanaume Aliyemtapeli Mpenzi Wake

RC Makalla Aingilia Kati Mgogoro wa Mwanaume Aliyemtapeli Mpenzi Wake June 8, 2021 by Denis MtimaMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla akizungumza.Baadhi ya madiwani kutoka Kinondoni wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.Taswira nzima ya Mkutano huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amewaonyesha kwa Vitendo Madiwani na Maafisa watendaji Kata namna ya kutatua migogoro inayowasumbua wananchi ambapo ametaka kila mtumishi  kuhakikisha anashughulikia kero za Wananchi.

Mgogoro wa kwanza aliotatua RC Makalla umehusisha Mwanamke mmoja aliedhulumiwa eneo na aliekuwa mchumba wake ambapo inasemekana Mwanaume huyo alitafuta Wakili na kufoji nyaraka za kuonyesha mwanaume huyo ni sehemu ya umiliki na uendelezaji wa eneo hilo ambapo Wakili ametumia Sheria ya Jiji la California nchini Marekani ambapo Mkuu wa Mkoa amekabidhi Jambo hilo kwa Vyombo vya vya dola kwaajili ya kulishughulikia kwa mujibu wa Sheria.

Aidha RC Makalla ametatua Mgogoro wa Mwananchi aliejenga Ukuta na kuziba Barabara za kuingia kwenye makazi ya watu ambapo amemuelekeza Afisa Ardhi Kinondoni kumaliza Mgogoro huo kwa kumuelekeza alieziba Barabara kuvunja na kuachia Barabara.

Pamoja na hayo RC Makalla amewapatia Madiwani na Maafisa watendaji Kata ajenda za kushughulikia ambapo miongoni mwa hizo ni kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Wananchi, Usafi endelevu wa Mazingira, Makusanyo ya Mapato na usikilizaji wa kero za Wananchi.

Agenda nyingine alizotoa RC Makalla ni usimamizi wa miradi ya maendeleo, Manispaa kutenga asilimia 10 ya mikopo kwa Vijana, Walemavu na Wanawake pamoja na kujenga umoja na mshikamano wa kazi miongoni mwa Watendaji na kuepuka Migongano na Mivutano.

Join our Newsletter