Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 24Article 573919

Habari Kuu of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

RC Makalla: Zinahitajika lita milioni 70 kumaliza tatizo la maji DAR, hali ni mbaya

RC Makalla: Zinahitajika lita milioni 70 kumaliza tatizo la maji DAR, hali mbaya. RC Makalla: Zinahitajika lita milioni 70 kumaliza tatizo la maji DAR, hali mbaya.

Wakazi wa Jiji la Dar es salaam wataendelea kukumbana na MGAO mkali wa Maji kwa muda mrefu kutokana na kuwa na upungufu wa Lita milioni 70.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ambae leo pamoja na Kamati nzima ya usalama ya mkoa wametembelea kukagua mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu juu na Ruvu chini.

Makala amesema kwa uzoefu wake akiwa Naibu Waziri wa Maji, uzalishaji wa Maji ni lita milioni 520 ambazo ndizo zinatosheleza kwa Jiji la Dar es Salaam ambapo vyanzo vikuu ni kutoka Ruvu Juu na Ruvu chini.

Amesema wakati maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yanatoka, kulikuwa na uzalishaji wa lita 65 lakini baada ya kudhibiti wavamizi imesaidia kuongezeka kwa lita milioni 200 na kufanya kuwa na upungufu wa lita milioni 70 kwa Ruvu chini.

Kwa upande wa upande wa Ruvu juu hali sio mbaya sana kutokana na uzalishaji wa maji kuendelea kuwa lita milioni 196 kwa siku.

"Baada ya kudhibiti wavamizi kwenye vyanzo vya maji kwa sasa maji yanayozalishwa ni lita milioni 200 bado hali sio nzuri, mgao wa Maji utaendelea kuwepo kwa muda mrefu tukisubiri kudra za Mwenyenzi Mungu mvua inyeshe , tulitegemea mvua za vuli lakii kukosekana kwa mvua hizo kwa takribani miezi miwili sasa imesababisha upungufu mkubwa na hali ikiwa hivi sijui itakuwaje, wananchi ingieni kwenye maombi" amesema Makala

Aidha kutokan ana hali hiyo, ametoa wito kwa Wananchi kutumia Maji vizuri na kuendelea kutunza vyanzo vya maji huku akipongeza jitiada zinazofanywa na na Dawasa.