Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 07Article 555808

Habari za Mikoani of Tuesday, 7 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

RC Makalla aahidi kukamilisha ujenzi mnada wa Pugu

Mnada wa mifugo wa Pugu Mnada wa mifugo wa Pugu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amesema atahakikisha kazi ya ujenzi wa eneo la mnada wa mifugo uliopo Pugu unakamilika kwa wakati ili uendane na mahitaji ya mifugo katika mkoa huo.

Makalla amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Mifugo Tanzania unaofanyika hii leo Septemba 07, 2021 kuwa, kutokana na mahitaji ya mifugo na uwepo wa machinjio ya kisasa ya mifugo Vingunguti, lazima kazi hiyo imalizike ili kupata mifugo iliyo bora Zaidi itakayo weza kushindana na soko la nje.

Wadau walioudhuria kikao hicho, wameongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, huku wakiwemo Wakuu wa Mikoa baadhi, na Wakuu wa Wilaya.

Hata hivyo, Mnada huo unatajwa kuwa wa kimatiafa, na utakapokamilika basi utawasaidia wafugaji kuweza kuuza mifugo yao kwa wepesi na haraka huku wakichangia kuinua pato la taifa.

Mara kadhaa Wizara ya Mifugo, imekuwa ikifanya jitahada katika kuhakikisha mnada huo unakamilika katika mudamuafaka na kwa viwango thabiti vilivyowekwa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matukio ya ubadhilifu yanayofanywa na viongozi baadhi wa mnada huo.