Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 26Article 540031

Habari za Mikoani of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

RC Mbeya awataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa uhuru  

RC Mbeya awataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa uhuru    RC Mbeya awataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa uhuru  

MKUU wa WIlaya ya Mbeya, Paul Mtinika amewataka wafanyabishara wa mkoa huo kufanya biashara zao kwa uhuru huku akiwataka wale wote wenye madeni ya kodi mikataba ya kuilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa awamu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Juma Homera, alipofungua Kikao cha mazungumzo kati ya TRA na Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Mbeya yaliyofanyika mapema leo katika Ukumbi wa jiji la Mbeya, Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wadau hao kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Mtinika amewata wafanyabiashara kutumia wakati huo kufanya mazungumzo na TRA ili waweze kuwekeana mkataba mzuri wa namna ya kulipa madeni yao ya kikodi kwa kuwa serikali ina nia njema ya kuwa karibu na wafanyabishara kwa kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na kurahisisha ulipaji kodi kwa njia ya mtandao.

“Serikali, kupitia mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, imewakaribia wafanyabiashara kwa kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na kuwaachia wafanyabiashara wafanye biashara zao kwa uhuru lakini hapo hapo watambue wajibu wa kulipa kodi kwa hiari,” amesema Mkuu huyo wa Wilaya

Aidha, amewataka wafanyabiashara wote wa Wilaya hiyo kushirikiana na TRA ili kuweza kutatua changamoto za kikodi zinazowakabili wafanyabiashara na hatimaye kulipa kodi ya serikali kwa mujibu wa sheria za kodi ambazo zimewekwa ili serikali ipate mapato ya kuwezesha maendeleo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema kuwa TRA, itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa walipa kodi ikiwemo kuanzisha mifumo ya kieletroniki inayowezesha wafanyabishara kulipa kodi zao kwa urahisi.

Kayombo ameongeza kuwa mikutano ya mara kwa mara kati ya TRA na wadau wake unalenga kuimarisha uhusiano pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kiutendaji zinazowakabili wafanyabishara ambapo kwa sasa mikutano hiyo itafanyika katika mikoa 19 ya Tanzania Bara.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabishara, Wenye Viwanda na Kilimo kitaifa Dk

Kulwa Kulwa alisema kwamba wafanyabishara wamepokea vizuri ujio wa mikutano hiyo kwa sababu inasaidia kuwaleta pamoja wafanyabishara wenye viwanda na kilimo na TRA na lengo lake ni kuzungumza, kuelimishana na kuweka mazingira ya ushirikiano kwa kuwa wote wanajenga nchi moja.

Join our Newsletter