Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 12Article 542350

Habari za Mikoani of Saturday, 12 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

RC Mwanza aeleza ziara ya Rais Samia

RC Mwanza aeleza ziara ya Rais Samia RC Mwanza aeleza ziara ya Rais Samia

Ziara hiyo itafanyika kwa siku tatu mkoani Mwanza na Rais Samia atapata fursa ya kuzindua mradi wa mtambo wa kuchenjua dhahabu uliopo eneo la Sabasaba jijini Mwanza.

Aidha, Rais Samia ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga, atakagua ujenzi wa daraja la JPM linalounganisha Kigongo-Busisi, atazindua mradi wa maji wilayani Misungwi na atazungumza na  vijana mkoani Mwanza siku ya mwisho ya ziara yake.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  Gabriel alitumia dakika chache kuzungumzia ziara ya rais na kisha kunyayuka na kuingia ofisini kwake na hapakuwa na maswali baada ya kutoa maelezo yake.

Hata hivyo, alichosema Gabriel kilishasemwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila jumatatu wiki hii alipokutana na waandishi wa habari.

Chalamila ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo, mapema asubuhi alikabidhi ofisi kwa Mkuu mpya  wa mkoa  ambaye amehamishwa kutoka mkoani Mara.